Tuesday, February 28, 2017

WAZIRI NAPE MGENI RASIMI FAINALI ZA ULEGA CUP ZITAKAZOFANYIKA MACHI 5 MKURANGA

Timu ya kata ya Tengelea, Tengelea FC  imefunzu kuingia katika fainali ya Ulega Cap baada ya kuifunga Timu ya Mwandege FC  bao 1 – 0 katika mcheezo uliochezwa jana katika viwanja vya shule ya Mkuranga jana .

Bao la timu ya Tengelea lilipatikana katika kipindi cha pili kupitia mchezaji  wao Andew Joseph aliyepokea cross ambayo ndio ilipa ushindi timu hiyo.
Timu ya kata ya Tengelea, itaingia fainali kwa kukipiga na timu ya Kisiju na mechi itanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu kati ya Mwandege FC na Lukanga FC.

Mgeni rasmi katika fainali za Ulega CUP ni Waziri Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa, Nape Nnauye.

Akizungumza na waandishi wa habari muandaji wa mashindano hayo Mbunge wa  Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa mashindano yameibua vipaji ya vipya.

Amesema kuwa inahitaji uwekezaji katika michezo kutokana na vijana kuonyesha vipaji vyao ambavyo vinatakiwa kuendelezwa.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Tengelea iliyopata ushindi wa kuingia fainali ya Ulega CUP katika mchezo uliochezwa jana katika viwanja vya shule ya Mkuranga jana.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mwandege ambao ni washindi wa tatu katika mashindano ya Ulega Cup baada ya kupata kichapo jana na timu ya Tengelea katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
  Vijana wakionyesha vipaji vyao katika mashindano ya Ulega CUP katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
 Mashabiki  wakiwa juu ya miti wakifatilia mpira kati ya timu ya Tengelea na Mwandege FC katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.

No comments: