Thursday, July 31, 2014

IPTL, Al-Madinah washerehekea sikukuu ya Eid na mayatima 500


Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta na wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak. 
 Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (kulia) na Meneja maswakla ya kampuni wa IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta (katikati) wakikabidhi sehemu ya bidhaa zilizonunuliwa wakati wa karamu ya chakula kwa watoto yatima wapatao 500 kutoka vituo mbali mbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa, kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak, ambao waliandaa karamu hiyo baada ya kufadhiliwa na IPTL. 
 Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta.
Meneja maswala ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kutoka vituo mbalimbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL.

ZAIDI ya watoto 500 wasio katika mazingira magumu na mayatima jijini Dar es Salaam na Wilayani Kondoa wameungana na waislam wengine duniani siku ya Jumanne kusheherekea sikukuu ya Eid, sikukuu inayoashiria kuisha kwa mwezi wa mfungo wa Ramadhani.

Watoto hao kutoka katika vituo mbali mbali vya watoto yatima, walipata fursa ya kula na kufurahia pamoja na wengine wakati wa karamu ya chakula cha watoto yatima ililoandaliwa na taasisi ya Ai-Madinah Social Service Trust na kudhaminiwa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Bw. Aidan Kaude, Meneja Rasilimali Watu wa IPTL aliejumuika na watoto hao jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe hizo alisema kampuni yake imeona haja ya kuisaidia Al-Madinah katika kuhakikisha kuwa watoto hao wanaohitaji msaada pia wanapata haki ya kusheherekea wakati huu muhimu katika maisha ya waislam wote dunia mzima.

"Tulipopata maombi toka Al-Madinah ili kusaidia kufanikisa karamu hii, Mwenyekiti wetu mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi aliidhinisha haraka ombi hilo na kusema kuwa ni jambo la kheri sababu watoto hao walengwa ni mayatima na wanahitaji msaada toka kwa kila mtu ili waweze kuishi maisha ya kawaida kama wengine wanavyoishi licha ya kupoteza wazazi wao," alisema.

Mkurugenzi wa Al-Madinah Social Service Trust, Sheikh Ally Mubarakí aliyeandaa tukio hilo alisema kuwa baada ya kufanyakazi karibu na kwa muda mrefu na makundi mengi na taasisi mbali mbali za kiislam, taasisi yake imegundua kuwa mayatima wengi wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na ukosefu wa mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi. 

Alisema taasisi yake iliomba msaada wa kifedha toka IPTL ili nao kuwapatia msaada wale watoto wenye maisha magumu, nafasi ya kusheherekea na waislam wenzao. Waislam walianza kusheherekea sikukuu ya Eid Jumatatu kwa dhehebu la Sunni na Jumanne kwa wengine, baada ya mwezi kuonekana na kuonesha mwanzo wa Shawwal, mwezi wa kumi wa Kalenda ya mwezi wa kiislama. 

Kuonyesha mwanzo wa Eid na kutoa Sunnah, kwa kuyafanya yake yaliyoganya na Mtume Muhammad, waislam wengi waliamka mapema kusali sala ya Asubuhi ya Sarat ul-Falr. 

Waslam wanasheherekea sikukuu kwa kukusanyika pamoja na marafiki na familia, na kuandaa vyakula vizuri , nguo nzuri kupeana zawadi na kupamba nyumba zao. Salaam ya kawaida wakati wa sikukuu hii ya Eid Madhubuti ya "Eid Mubarak" ikimaanisha "uwe na Eid iliyo na upendo."

No comments: