Tuesday, April 29, 2014

Wanamichezo 45 waagwa rasmi kwa ajili ya kwenda nje kufanya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akizungumza na wanamichezo wanaoenda kuweka kambi katika nchi za New Zealand, Ethiopia, China na Uturuki ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola mapema mwezi julai. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leornard Thadeo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leornard Thadeo akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuwakabidhi bendera wanamichezo wanaokwenda nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya njeya nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wa tatu kutoka kushoto) akifurahia mara baada ya kuwa kabidhi Bendera ya Taifa wawakilishi wa wanamichezo wanaokwenda nchini New Zealand, Ethiopia,China na Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na msahindano ya Jumuiya ya Madola. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Asia, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leornard Thadeo, Katibu wa Kamati ya Olympic Tanzania Filbert Bayi na mwakilishi wa wana michezo Neema Mwaisyula.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania Anthony Mtaka akitoa neon la shukrani kwa niaba ya wanamichezo wote wanaoshiriki maandalizi hayo.
Baadhi ya wanamichezo na viongozi wao wakifuatilia kwa karibu hotuba ya Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuwakabidhi Bendera ya Taifa leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Leornard Thadeo akipeana mkono na mwakilishi wa wana michezo wanaoenda nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa wa Mambo ya nje ya nchi na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (mwenye shati la njano)
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akiwa na mchezaji wa timu ya Taifa ya kuogelea Hilal Hemed Hilal. PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA

No comments: