Thursday, November 29, 2012

AMANA BANK YAZINDULIWA RASMI


Amana Bank inajivunia kuwa benki ya kwanza kabisa ya Kiislam nchini Tanzania ikiwa na malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee ambazo zinafuata Sharia kikamilifu kwa kuzingatia maadili na kwa njia iliyowazi na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wateja wetu wote.

 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Amana Bank,                             
Bw. Haroon Pirmohamed akitoa historia fupi ya benki alisema, “Historia ya kuanzishwa kwa Amana Bank, inaanzia mwezi October mwaka 2009 ambapo baadhi ya wafanyabiashara walikutana na kupanga mikakati ya kuanzisha benki ya kiislam nchini Tanzania isiyofuata misingi ya riba. Benki ilipata leseni ya muda kutoka Benki Kuu ya Tanzania tarehe 4 Februari 2011 na kusajiliwa rasmi tarehe 25 Februari 2011 ikiwa na mtaji ulioidhinishwa wa Shilingi za Kitanzania Billioni 100 na uliolipiwa kiasi cha shilingi za kitanzania Billioni 21.5”.

Aliendelea kusema kuwa, “katika mwaka mmoja Amana Bank imeweza kufungua matawi matatu jijini            Dar es Salaam. Matawi hayo ni Tandamti lililoko eneo la Kariakoo, Nyerere Road Branch, lililopo barabara ya Nyerere na Main Branch lililopo katikati ya jiji katika jengo la Golden Jubilee Tower”.

Benki inatoa huduma na bidhaa ambazo zinafuata misingi ya Sharia za kiislam na ambazo zimepitishwa na Bodi ya Sharia. Bidhaa na huduma zinazotolewa na benki si kwa ajili ya jamii ya kiislam pekee bali kwa watu wote ambao wanaamini katika mfumo wa kibenki usiofuata misingi ya riba. Huduma za Amana zinatolewa kwa makampuni na watu binafsi. Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-

Akaunti za Akiba ambazo zinajumuisha Akaunti ya watoto (Nuru Akaunti), Akaunti ya wanawake (Annisa Akaunti), Akaunti ya akiba kwa ajili ya nyumba za ibada zilizosajiliwa (Ihsan Account) pamoja na Akaunti ya Hijja (Hajj Account). Pia benki ina Akaunti za hundi na Akaunti za biashara. Vilevile benki ina akaunti ambazo ni maalum kwa ajili ya makampuni mbalimbali. Benki pia ilianzisha huduma ya ulipaji wa kodi za mapato na ushuru wa fordha kupitia matawi yake. Wateja na wasio wateja sasa wanaweza kulipa kodi hizi katika matawi ya Amana Bank. Pia benki ilianzisha huduma ya kutuma fedha popote duniani kupitia huduma ya Western Union. Benki ina lengo la kumfanya mteja  anapoingia katika matawi yetu apate huduma zote mahali pamoja (one-stop shop).

“Mpaka tarehe 25 Novemba mwaka huu, Amana imefanikiwa kuwa na jumla ya akaunti 4093 na akiba zaidi ya Shilingi Bilioni 35”, alisema Mwenyekiti Bw. Haroon Pirmohamed.

Ni kwa kutumia teknolojia hii ya kisasa Amana Bank ilizindua huduma ya Amana Mobile ambayo inaenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia duniani. Amana Mobile ni huduma za kibenki kwa kutumia mtandao wa internet na simu za mkononi.”  “Huduma hii inalenga kuwarahisishia wateja wetu kufanya miamala na kupata huduma mbalimbali ambazo zinatolewa  na benki yetu kwa  njia ya mtandao.  Lengo la kuanzisha huduma hii ni kurahisisha usimamizi wa akaunti za wateja wakati wowote, popote walipo siku saba za wiki” alisema mwenyekiti.

Kwenda mbele, uongozi wa benki unafanya jitihada kubwa kuboresha nafasi ya benki katika soko na pia kusambaa sehemu nyingine nchini. Benki inatarajia kufungua matawi matatu mwanzoni mwa mwaka 2013 katika mikoa ya Arusha na Mwanza na tawi la pili katika eneo la Kariakoo mtaa wa Lumumba. Pamoja na ufunguzi wa matawi, Amana Bank pia inajipanga kuboresha huduma zake na pia kuongeza huduma zingine.

Tunawakaribisha wote kufungua akaunti Amana Bank. Karibuni katika ulimwengu mpya kabisa wa kibenki, unaofuata Sharia kikamilifu.
Kwa maelezo na taarifa zaidi unaweza kupata kupitia tovuti  yetu ya www.amanabank.co.tz

No comments: