Sunday, November 27, 2011

MKUTANO WA KIHISTORIA KATI YA RAIS KIKWETE NA UONGOZI WA CHADEMA IKULU DAR ES SALAAM LEO NOVEMBA 27, 2011

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo toka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe baada ya kupokea  mapendekezo ya chama hicho juu ya kuundwa katiba mpya yatayozungumzwa kwenye mkutano huo wa kihistoria uliofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa CHADEMA katika mkutano huo wa kihistoria
 Mkutano ukiendelea 
 Rais Jakaya Kikwete akiongea na uongozi wa CHADEMA (kushoto) pamoja na ujumbe wa Serikali (kulia)
 Mh. Tundu Lissu akikoroga chai baada ya mkutano huku Profesa Baregu naye akijiandaa kujisevia
 Rais Jakaya Kikwete akimpa juisi Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe baada ya mkutano
 Rais Jakaya Kikwete akiongea na wageni wake kwa bashasha baada ya mkutano
 Rais Kikwete na wageni wake wakilegeza makoo baada ya masaa mawili na nusu ya mkutano
 Rais Jakaya Kikwete akiongea na wageni wake
 Furaha ilitawala baada ya kumalizika kwa mkutano na wageni kuinuka na kuaga
 "....Asante sana Mh Rais kwa kukubali mwaliko wetu..." anasema Mh Freeman Mbowe wakati akiaga
 Mh Arfi akiaga
 Kaimu Katibu Mkuu Mh John Mnyika akiaga. Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa alitoa udhuru kuwa unauguliwa hivyo hakuweza kufika
 Mh Mrema akiaga
 Kwaheri Mheshimiwa na asante kwa kutukaribisha Ikulu...
 Profesa Mwesiga Baregu akiaga
 Profesa Abdallah Safari akiaga
 Mh Tundu Lissu akiaga
Mh Tundu Lissu akiondola Ikulu taratibu baada ya mkutano huku gari iliyombeba mwenyekiti wa CHADEMA ikiondoka pia...

5 comments:

Muddy Nice said...

Hi Mithupu,
This is wonderful, yaani ukimuona Kikwete usoni anaonyesha kabisa kuwa anataka kitu chema na kizuri, rais anataka mabadiriko ila tatizo linakuja kwa wasaidizi wake, wao wako kimbele mbele kumsemea Kikwete na kujipendekeza kwake kwa kukataa kila jambo linaloanzishwa na watu wa upinzani hata kama ni zuri kiasi gani. Sasa kikowapi kilichoamliwa na kamati kuu ya CCM, walichomwambia eti asikutane na Chadema bali akutane na vyama vyote kwa pamoja!!!!, jamani ni Chadema ndio walioomba kukutana na Kikwete na sio wote.

Kikwete big up sana, mimi najua wewe una nia ya dhati ya kuliendeleza ili taifa ila tatizo wapambe wako ndio kikwazo kikubwa kwako kuendelea. BIG UP MKUU WA NCHI YANGU. Kwakweli kwa mala yangu ya kwanza nimekuona ukitumia busara ya hali ya juu. Ona sasa kikao kimekwisha na kila mtu amefurahi, je ingekuwaje endapo ungekataa kukutana nao au endepo ungefuata mawazo mgando na uliowachagua ya kukutaka ukutane na vyama vyote?, si yangetokea marumbano yasiyokuwa na mbele wala nyuma. Asante sana kwa kutumia busara zako.

Muddy Nice

Anonymous said...

Wanandugu na wapenzi wa nchi yetu.Ya muhimu katika hili si ushabiki wa mambo bali ni kuzingatia yale yatakayoendeleza upendo amani na haki.Tanzania tunataka maendeleo,na tunataka usawa,pia ufujaji wa mali za umma usitishwe.Katiba ijayo uyaainishe hayo na kuwapa watu na wana wa nchi haki.

Mungu mbariki kila aitakiaye nchi hii kheri.Ameen

Anonymous said...

ni tukio zuri ambalo litaleta makubaliano,nampongeze Rais JK kwa kukubali ombi la chadema.
By Best

Ole Lotashu said...

Mungu ibariki Tanzania na viongozi wote!!!! CCM IJALI NA ISIKILIZE WANACHOSEMA WAPINZANI KWANI WAMECHUGULIWA NA WATANZANIA KAMA WAO, HONGERA KIKWETE NA USISIKILIZE USHAURI M BAYA KWA KUSHINIKIZWA NA WALIO CHINI YAKO. TUNAKUPENDA NA TUTAENDELEA KUKUPENDA KAMA HUTAPOTEZA AMANI NA MSHIKAMANO WETU TULIOACHIWA NA BABA WA TAIFA.

Anonymous said...

Asante mh.Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania kwa kuonyesha mfano mzuri,kuwa Tanzania ni nchi ya demokrosia ya kweli na ni nchi ya amani.Kwa kukubali kuongea na chama cha upinzani ikulu.

Pia pongezi kwa ujumbe wa Chadema ukiongozwa na mwenyekiti wake Mh,Mbowe kwa kuonyesha ari ya kuifanya nchi yetu iwe pahala pa amani kwa kuheshimu mazungumuzo na serikali tawala.Mungu ibariki Tanzania na watu wake.